Lyrics
Na wala sio sababu ya jina langu
Wala sio sababu ninafaa
Najua sio sababu ya sadaka zangu
Maana ndio bado nina shangaa
Nilijua kwamba nimeshapoteza nafasi
Mimi ni nani kwani nakosa neno kusema
Ooh unisamehe, sikujua unanipenda hivi
Umefanya bure, sawa na upendavyo
Ume ruhusu niwe vile upendavyo
Nitakushukuru tu, kwa neema
Asante tu, kwa wema
Ninakushukuru tu, kwa neema
Asante tu, kwa wema
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Wacha machozi
(Wacha machozi yanitiririke tu)
Yanitiririke
(Wacha kilio, nikulilie Mungu)
Basi wacha machozi
(Wacha machozi, yanitiririke tu)
Wacha kilio
(Wacha kilio, nikulilie Mungu)
Natafuta cha kunitenga nawe
Bado sijaona
Nilisha katwakatwa moyo
Na kupondwa na wanadamu
Leo wataniambia nini, nikiwa nawe
Leo wata niambia nini uuh uuuh, nikiwa nawe
Pesa huitwa sabuni ila maji niwe
Unioshe bwana, nitakase
Nitakushukuru tu, kwa neema
Asante tu, kwa wema
Ninakushukuru tu, kwa neema
Asante tu, kwa wema
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Maana kama si wewe
(Kama si wewe, ningekua wapi)
Wacha machozi
(Wacha machozi yanitiririke tu)
Wacha kilio
(Wacha kilio, nikulilie Mungu)
Wacha machozi
(Wacha machozi, yanitiririke tu)
Wacha kilio
(Wacha kilio, nikulilie Mungu)