Lyrics
Umeahidi wewe bwana… huniachi
Hadi mwisho wa dahari ulisema huniachi
Wewe ni mungu uliye mwaminifu siku zote
Mimi ninaiweka imani yangu kwako baba
Unalijua jina langu ewe bwana… huniachi
Unatengeneza njia hata mito kule jangwani
Wewe ndiwe alpha na omega… huniachi
Ukamtoa danieli kutoka tundu la simba
Wewe huwainua na wanyonge siku zote
Watuepusha na hatari kila siku usifiwe
Marafiki nao wanaweza nigeuka
Mara kwa mara maadui wanizunguka
Nitaishi kwa ahadi yako bwana, huniachi huniachi